Michakato ya Usomaji Miswada
Makala zote zinazochapishwa na Jarida hili zinapitiwa kwa kina na mhariri katika awamu ya kwanza, kisha zikikidhi vigezo, husomwa na kufanyiwa tathmini na wasomaji-fiche. Mchakato wa usomaji wa mswada unatumia kuanzia mwezi mmoja hadi miezi minne hadi mswada utakapokubaliwa kuchapishwa. Kwa kuwa wasomaji-fiche wetu wengi wanajitolea, mchakato wa usomaji miswada unaweza kuchukua muda mrefu zaidi lakini haiwezi kuzidi miezi mitano. Kwa nadra sana, mchakato wa usomaji unaweza kuchukua hadi miezi 6 bila mawasiliano na mwandishi kuhusu ugumu uliojitokeza.