DHIMA YA MSIMULIZI KATIKA RIWAYA YA DUNIA UWANJA WA FUJO
Abstract
Hadithi yoyote husimuliwa. Usimulizi huo hufanywa na msimulizi ambaye kwa hakika huwa tunaisikia sauti yake. Hata hivyo, katika kazi za fasihi andishi kama vile riwaya, sauti ya msimulizi huwa haisikiki kwa masikio kama ilivyo katika usimulizi wa simulizi za kimapokeo, bali wasomaji huweza kuisikia kwa kutumia akili zao wanapoisoma kazi husika (Mohochi, 2000). Sauti hii ya msimulizi inayosikika katika akili za wasomaji huwawezesha kubaini anayeongea na dhima anayoitekeleza katika kazi husika. Hivyo, makala haya yamejikita katika kubainisha dhima za msimulizi katika riwaya ya ' Dunia Uwanja wa Fujo ' ya Euphrase Kezilahabi.