FASIHI YA WOTOTO KATIKA KUTEKELEZA MAHITAJI YA MTOTO KISAIKOLOJIA
Abstract
Lengo la makala haya ni kubainisha umuhimu wa fasihi ya watoto katika kutekeleza mahitaji yao kisaikolojia. Katika kufanya hivi tumezingatia masuala mbalimbali yanayohusu sifa bainifu za watoto pamoja na kujadili vipengele muhimu katika fasihi ya watoto na kuonesha jinsi vinavyochangia katika kumnufaisha mtoto kisaikolojia.