' Unapoteza wakati wako bure! Hakuna atakayekuamini ' : Usawiri wa Ubakaji katika Riwaya Teule za Kiswahili

Authors

  • Ernesta S. Mosha University of Dar es salaam

Abstract

Makala haya yanajadili tatizo la ubakaji kama lilivyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili. Kwa kutumia kilongo cha ashiki ya kujamiiana, makala yanaweka wazi mbinu mbalimbali zinazotumiwa na waandishi na kuwafanya wabakaji kuonekana kuwa hawana makosa huku wanawake wanaobakwa wakibebeshwa lawama kutokana na unyanayasaji wanaopata. Mwandishi wa makala anaeleza kuwa usawiri wa aina hii unaendeleza unyanyasaji wa wanawake na unarudisha nyuma juhudi za jamii katika kuleta usawa wa wanawake na wanaume. Athari kubwa inayoweza kutokana na usawiri huu ni kuhalalisha unyanyasaji wa wanawake katika jamii inayolea na kuendeleza vitendo hivi vya kinyanyasaji. Aidha, makala yanabainisha kuwa riwaya zinaweza kutumika katika harakati za kupambana na tatizo hili la ubakaji kwa kusawiri mbinu zitakazowasaidia wanajamii kukomesha ubakaji pamoja na kukosoa vilongo vinavyoendeleza ubakaji kwa kuchomoza na kushadidia vilongo mbadala vinavyowaelimisha wanajamii namna wanavyoweza kuunga mkono harakati za kutokomeza aina hii ya unyanyasaji katika jamii ya Tanzania.

Author Biography

Ernesta S. Mosha, University of Dar es salaam

Mwalim

Downloads

Published

2016-02-15

Issue

Section

Articles