Vipengele vya Sanaa za Maonyesho za Kiafrika katika Tamthiliya za Kiswahili kama Mbinu ya Uibuzi wa Dhamira

Authors

  • Elizabeth Godwin Mahenge University of Dar es salaam

Abstract

Msingi wa kufanya utafiti wa makala hii unatokana na msukumo alioupata mtafiti wa kutaka kuchunguza ili kuona kama kuna kitu tunaweza kukiita "tamthiliya ya Kiswahili ya Kiafrika" katika tamthiliya za Kiswahili zilizopo Tanzania na Kenya. Makala imetumia jina hilo ili kujitofautisha na "tamthiliya za Kiaristotle" ambazo zipo kwa kiasi kikubwa katika fasihi ya Kiswahili. Methodolojia iliyotumika ili kuipata data ilikuwa ni uchambuzi wa kifasihi ambao ulijumuisha kuisoma tamthiliya tangu mwanzo hadi mwisho na kuweka alama katika vipengele vya sanaa za maonesho vilivyojitokeza. Matokeo ya uchambuzi huu yamebainisha kuwa, kuna utajiri mkubwa wa vipengele vya sanaa za maonesho katika tamthiliya za Kiswahili tulizozichambua. Hivyo, matumizi ya vipengele vya sanaa za maonesho ya Kiafrika katika tamthiliya za Kiswahili yanatuthibitishia kuwapo kwa "tamthiliya ya Kiswahili ya Kiafrika" ambayo ndiyo hoja mojawapo iliyomsukuma mtafiti akaandika makala hii japokuwa hoja nyingine zitatajwa katika sehemu ya utangulizi.

Published

2016-02-12

Issue

Section

Articles