Usawiri wa Mwanamke Mchawi katika Riwaya za Kiethnografia za Kiswahili
Authors
Lameck Mpalanzi
University of Dar es salaam
Abstract
Usawiri wa mwanamke katika fasihi umechunguzwa na wanazuoni mbalimbali. Tafiti zilizopo zinamuonesha mwanamke kama mzazi, chombo cha kuzalisha mali, chombo cha anasa, mtu asiye na uhuru na/ama mfanyakazi wa nyumbani. Kwa upande mwingine, tafiti chache zinachunguza mwanamke kwa jicho la kianthropolojia na kifalsafa. Kwa mfano, Mekacha (1993) anamlinganisha mwanamke sawa na ibilisi/shetani kwa kuwa anatazamwa kama chanzo cha maovu yote. Naye, Mesaki (1993) anachunguza namna mwanamke anavyobeba tajiriba za kichawi katika jamii nchini. Anaona kuwa wanawake vikongwe wanauawa zaidi kutokana na tuhuma za uchawi. Mwandishi wa makala hii anachochewa na fikra za Mekacha (khj) na Mesaki (khj) na hatimaye anachunguza namna uchawi wa mwanamke unavyojitokeza katika riwaya za kiethnografia za Kiswahili. Makala hii inalenga uchambuzi wa riwaya nne za kiethnografia za Kiswahili. Makala inabainisha kuwa ijapokuwa wanawake na wanaume wanaweza kuwa wachawi, wanawake wana mamlaka zaidi katika magenge ya wachawi. Kadhalika, wanawake ndiyo wateja wakuu, washirika wakuu, washauri na wahanga katika masuala yanayohusu uchawi. Aidha, mambo yanayowafanya wanawake kujihusisha na uchawi ni changamoto za kisaikolojia, kijinsia na kiontolojia.