Ulinganishi wa Ngeli za Nomino za Lugha za "RunyaÄitara"1
Authors
Asiimwe Caroline
University of Dar es salaam
Abstract
"RunyaÄitara" ni lugha zinazozungumzwa Magharibi mwa Uganda na zina uhusiano unaofanya baadhi ya wanazuoni kuhisi kwamba ni lahaja za lugha moja. Makala hii inahusika na ulinganishi wa ngeli za nomino za lugha zote nne za "RunyaÄitara". Ulinganishi wa ngeli za nomino katika lugha hizi umefanywa kwa kuegemea namna maneno yanavyojitokeza kwa kuzingatia viambishi, maana na dhima za viambishi hivyo katika lugha hizi. Makala inafafanua kwamba uainishaji wa ngeli za nomino unaweza kufanywa kwa kuegemea mikabala tofautitofauti kulingana na wanazuoni tofauti. Hata hivyo, ulinganishi wa lugha za RunyaÄitara kwa kuegemea mikabala hiyo umeonesha kwamba lugha hizi zina mfanano wa hali ya juu - hali inayoonesha kwamba zina uhusiano wa karibu.