Shujaa wa Kike1 katika Bunilizi za Kihistoria za Watoto katika Kiswahili
Authors
L. H. Bakize
University of Dar es salaam
F. E.M.K. F.E.M.K. Senkoro
Chuo Kikuu Cha Dar es salaam
Abstract
Tafiti nyingi zilizofanyika katika fasihi ya Kiswahili kwa nyakati tofauti, iwe ni katika fasihi simulizi au andishi, zinaonesha kwamba mwanamke amechorwa kama kiumbe duni na dhaifu katika jamii. Hata hivyo, pamoja na hoja hizo za watafiti, utafiti wetu umeonesha kwamba bunilizi za kihistoria za Kiswahili, zilizoandikwa kwa ajili ya kusomwa na watoto, zinamchora mtoto wa kike kama shujaa anayeweza kupambana na kukabiliana na kila hali kama mvulana. Makala hii imeshughulikia masuala makuu mawili: Mosi, kazi teule za kihistoria za watoto zilizomchora kama shujaa; pili, kufafanua sababu za waandishi wa bunilizi hizo za kihistoria kumsawiri mtoto wa kike kama shujaa. Makala imeandikwa kwa mkabala wa ujenzi wa dhana ya utaifa. Dhana ya utaifa ilitumiwa na waandishi baada ya kuonekana kutawala katika kazi zilizochambuliwa. Makala hii imeongozwa na Nadharia za Mwitiko wa Msomaji na Uchanganuzi nafsi. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba waandishi wa bunilizi wana fursa ya kuumba ulimwengu wanaoutaka kupitia kazi zao; wanaamini kuwa ili ujenzi wa taifa ufanikiwe kwa haraka, wanawake na wanaume wanapaswa kushirikiana bila kujali jinsi zao; na mwisho, wanaonekana kuamini katika kuibadilisha jamii badala ya kuilaumu kimtazamo kuhusiana na masuala ya ujinsia kwa kumdunisha mwanamke.
Author Biographies
L. H. Bakize, University of Dar es salaam
Mwalim
F. E.M.K. F.E.M.K. Senkoro, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam