Matumizi ya Thieta ya Kiutendi katika Tamthilia za Ebrahim Hussein: Kinjeketile (1969), Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi (1976)

Authors

  • Sophie Okwena University of Dar es salaam

Abstract

Ebrahim Hussein ni miongoni mwa waandishi wakongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kuishi kwake na kuingiliana na tamaduni tofauti kumemfanya achukue vipengele vya tamaduni hizo na kuvifanya kuwa vipengele muhimu katika maisha yake na katika kazi zake za kiubunifu. Isitoshe, mwandishi huyu hajajifunga katika utambulisho mahususi. Hivyo, Hussein anashirikisha miundo ya kidrama ambayo ilichimbuka kutokana na usomaji wa maandishi tofautitofauti. Aidha, sifa katika uandishi wake ni pana ambazo zingine zimetokana na mapokeo ya Kimagharibi kama vile ya Ki-aristotle na dhana yake ya tanzia, Hegel katika masuala ya kipembuzi, na thieta ya ki-utendi kutoka kwa Brecht. Hussein alisomea Shahada yake ya Uzamivu katika Sanaa za Maonesho na Historia nchini. Ujerumani. Kwa hiyo, maisha yake ya kitaaluma pamoja na yale ya kukua kwake katika nyakati za ukoloni bila shaka yameathiri uandishi wake kwa namna tofauti kama inavyodhihirika katika tamthilia zake. Mawazo ya Hussein hayajikiti katika ' Uswahili ' au ' Uafrika ' maalumu bali   ameyachota kutoka visima tofauti vya Kiafrika na Kimagharibi.

Author Biography

Sophie Okwena, University of Dar es salaam

Mwalim

Published

2020-02-29

Issue

Section

Articles