Uchi kama Mkakati wa Kulipiza Kisasi katika Muziki wa Kizazi Kipya: Mfano wa Wimbo wa "Kwangwaru" wa Harmonize na Diamond Platnumz

Authors

  • Fred Wanjala Simiyu Chuo Kikuu cha Kibabii, Bungoma, Kenya.

Abstract

Dhana ya uchi inajitokeza katika nyanja mbalimbali katika jamii zote ulimwenguni, hasa katika fasihi pendwa kama vile nyimbo za kizazi kipya zinazoshabikiwa zaidi na vijana. Kadhalika, suala la kisasi limeangaziwa katika fasihi za jamii mbalimbali kama vile mashairi ya Iliad yaliyoandikwa na Homer, tamthilia ya Hamlet iliyoandikwa na William Shakespeare na ile ya Oedipus iliyoandikwa na Sophocles. Hata hivyo, suala hili la uchi ' halipaswi kutajwa ' katika jamii nyingi kwa sababu ni mwiko. Kumbe, fanani vijana wanatumia TEHAMA kama jukwaa maalumu la kuendeleza uvunjaji wa miiko hiyo ili kuwasilisha ujumbe mahususi. Makala hii inalenga kubainisha matumizi ya uchi katika kuwasilisha masuala ya kisasi katika nyimbo za kizazi kipya kwa kutumia wimbo wa "Kwangwaru" ulioimbwa na Harmonize na Diamond Platnumz kama mfano. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Kisasi inayoshikilia kwamba kisasi ndiyo motisha kuu ya kila tunachofanya katika maisha yetu ya kila siku japo hatutaki kuamini.

Published

2021-04-21

Issue

Section

Articles