Kifo na Hofu katika Ua la Faraja

Authors

  • Matthew Kwambai Chuo Kikuu cha Egerton, Nakuru, Kenya.
  • Abdulrahim H.T. Ali Chuo Kikuu cha Egerton, Nakuru, Kenya.
  • Issa Mwamzandi Chuo Kikuu cha Egerton, Nakuru, Kenya.

Abstract

Binadamu anapojikuta duniani kwa kukosa uwezo wa kuchagua uwepo wake, hukumbana na changamoto mbalimbali zinazotokana na matendo anayoyafanya. Katika kutafuta suluhu ya changamoto anazokumbana nazo, binadamu hujiingiza katika masuala tofauti kama vile dini, ulevi, ngono na kadhalika. Anapokosa suluhu ya matatizo yake, huamua kukabiliana na kifo kama njia ya kujipumzisha. Makala hii inakusudia kuangazia kifo na hofu ya wale wanaozunguka waliofiwa na matokeo yake katika riwaya ya Ua la Faraja. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ya Udhanaishi. Nadharia hii inaangazia uwepo wa binadamu duniani, matatizo anayopitia, utafutaji wa uhuru na mwisho kifo kama suluhu. Uchanganuzi wa yaliyomo katika riwaya ya Ua la Faraja na makala mbalimbali kwenye maktaba na mtandao ulifanywa ili kuelewa dhana ya kifo na hofu. Utafiti huu ulichunguza vifo vya wahusika watatu: Ngoma, Tabu na Queen pamoja na mitazamo ya wahusika Omolo na Dkt. Hans. Kilichobainika ni kuwa kifo kiliwatisha wahusika waliokuwa wakisubiri kufariki dunia na vilevile, kiliwahuzunisha wafiwa.

Published

2021-04-21

Issue

Section

Articles