Maandishi ya Kijamiilughaulumbi katika Mandharilugha ya Jiji la Dar es Salaam:Aina zake na Mdhihiriko wa Taarifa za Kiisimujamii

Authors

  • Rhoda Peterson Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam, Tanzania

Abstract

Matumizi ya wingilugha yanazidi kuongezeka katika mandharilugha ya miji mbalimbali ulimwenguni. Kutokana na ongezeko hilo, ni hali ya kawaida kuona maandishi ya kijamiilughaulumbi katika eneo la mandharilugha. Katika nchi ya Tanzania kwa mfano, tafiti zinadhihirisha kuwapo kwa maandishi ya kijamiilughaulumbi kwenye miji kama vile Dar es Salaam, Arusha, Iringa, Kagera, Manyara na Mbeya. Aidha, maandishi ya kijamiilughaulumbi katika mandharilugha yanaweza kuwa katika aina tofautitofauti kutegemeana na jamiilugha husika. Lengo la makala hii ni kuchunguza aina za maandishi ya kijamiilughaulumbi katika mandharilugha ya jiji la Dar es Salaam kwa kutumia mkabala wa Reh (2004) na kubainisha taarifa za kiisimujamii zinazodhihirishwa na aina hizo. Data zilikusanywa katika maeneo ya Posta na Kariakoo jijini Dar es Salaam. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwapo kwa aina za ujalizaji pamoja na urudufishaji usofumbato. Pia, uchanganyaji wa lugha kwa kiasi kikubwa umehusisha Kiswahili na Kiingereza ambazo ni lugha rasmi nchini Tanzania huku lugha nyingine (Kiarabu, Kihindi na lugha za asili) zikitumiwa kwa kiasi kidogo.

Published

2021-04-21

Issue

Section

Articles