Dosari za Kimatamshi Zinazojitokeza katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili kwa Wanafunzi wa Jamiilugha ya Kihaya

Authors

  • Deodatus Rutagwerela Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Abstract

Makala haya yanachunguza dosari za kimatamshi zinazofanywa na wanafunzi wa jamiilugha ya Wahaya wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili katika shule za msingi za Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera. Data ilikusanywa kupitia insha na masilimulizi ya wanafunzi. Aidha, njia ya hojaji ilitumika kupata taarifa kuhusu dosari kutoka kwa walimu kutokana na uzoefu wao wa kufundisha Kiswahili kama somo. Nadharia ya Usasanyuzi Dosari iliongoza utafiti kwa kuzingatia msingi mkuu wa kuchambua dosari kutokana na utendaji wa mjifunzaji. Uchambuzi wa data unadhihirisha kuwa wajifunzaji walifanya dosari za: ubadilishanaji, udondoshaji pamoja na uchopekaji wa fonimu tofauti na kaida za michakato ya matamshi ya Kiswahili sanifu. Dosari za matamshi zilizobainishwa zimesababisha wajifunzaji kushindwa kutumia Kiswahili sanifu na fasaha kufanikisha malengo yao kimawasiliano. Makala yanabainisha kuwa, kutokana na wajifunzaji kuwa katika kipindi faafu, dosari zilizojidhihirisha zinaweza kurekebishika kwa kiasi kikubwa iwapo tu nadharia na kaida za ufundishaji wa lugha ya pili zitazingatiwa. Makala haya yanahusisha sehemu ya data iliyokusanywa katika utafiti wa kuandaa tasnifu ya uzamivu (2018).

Author Biography

Deodatus Rutagwerela, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Mwanafunzi wa Uzamivu 2021

Published

2022-04-14

Issue

Section

Articles