Matamshi na Tahajia ya Istilahi Mkopo za Kiingereza katika Kiswahili: Mifano kutoka Istilahi za Sayansi Ikisiri

Zabron T. Philipo

Abstract


Lengo la makala haya ni kuonesha ruwaza ya matamshi na tahajia ya Istilahi Mkopo (kuanzia sasa IM) za Kiingereza zinazoingizwa katika Kiswahili. Mtazamo wa asasi zinazohusika na uundaji istilahi kama vile Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kuhusu matamshi na tahajia ya IM unaonesha kuwa IM zenye matamshi kama yalivyo katika Kiswahili na kuwa na tahajia ya IM zenye muundo wa maandishi kama ilivyo katika Kiingereza. Data na hoja zilizowasilishwa katika makala hii zimetokana na hojaji, usaili na upitiaji nyaraka[1]. Hivyo, data hizo zinadhihirisha kuwa kuna uhalali wa kuangalia upya ruwaza ya matamshi na tahajia ya IM za Kiingereza katika Kiswahili. Makala haya yanabainisha kuwa IM ziwe na ruwaza ya matamshi kama ilivyo katika Kiingereza. Kwa mfano,  <hydrogen> - /haidrojeni/ na tahajia iwe ni ile ya muundo wa matamshi badala ya ule wa maandishi. Kwa mfano, <hydrogen>- <haidrojeni> *<hidrojeni>. Makala yanatoa mwongozo wa matamshi na tahajia ya IM katika Kiswahili.


[1]Data na hoja za makala haya  zimetokana  na tasnifu yangu wa Udaktari wa Falsafa - PhD (2018).


Full Text:

 Subscribers Only

Refbacks

  • There are currently no refbacks.