Mtazamo Linganishi wa Muundo na Maudhui ya Tenzi Mbili za Kale na Ushairi wa Muyaka

Authors

  • Jessee Murithi Chuo Kikuu cha Kenyatta

Abstract

Fasihi huelezea kuhusu matukio katika jamii. Kazi hizi huweza kuiga miundo, mitindo na maudhui ya kazi za awali. Kuiga huku huweza kufanya kazi hizo kuwa na vipengele vinavyofanana na kazi zilizotangulia. Kwa sababu hii, makala haya yanalenga kulinganisha miundo na maudhui ya tenzi mbili za kale za lugha ya Kiswahili na ushairi wa Muyaka Bin Haji. Tenzi hizi ni: Utendi Al-Inkishafi na Utenzi wa Liyongo. Uchanganuzi huu utaonesha ikiwa kuna sifa za kimuundo na kimaudhui zinazofanana katika tenzi hizi na pia kutofautiana, hasa ikizingatiwa kuwa watunzi wa tenzi hizi walitunga katika kipindi kimoja na Muyaka Bin Haji. Nadharia iliyoongoza uchanganuzi huu ni nadharia ya "Ukae" (Classicism) ambayo ina mihimili kama ukale wa msamiati, ubunifu wa kiwango cha juu, kurejelewa na wasanii wengine katika enzi tofauti kati ya mingine.

Author Biography

Jessee Murithi, Chuo Kikuu cha Kenyatta

Mhadhiri, Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Kenyatta, Nairobi, Kenya

Published

2022-04-14

Issue

Section

Articles