Falsafa ya Kiafrika katika Tendi za Kiafrika: Mifano kutoka Utenzi wa Nyakiiru Kibi (1997)
Abstract
Lengo la makala haya ni kuchunguza ujitokezaji wa vipengele vya falsafa ya Kiafrika katika tendi za Kiafrika. Utendi unaochunguzwa ni Nyakiiru Kibi (Mulokozi, 1997). Utendi huu umechunguzwa kwa kutumia Nadharia ya Ontolojia ambayo imetusaidia kuchambua vipengele vya falsafa ya Kiafrika. Tendi kama zilivyo tanzu nyingine za fasihi, zinaweza kubeba mitazamo, imani, itikadi, mwelekeo na uhalisia wa jamii husika. Makala yamebaini kuwa tendi zinabeba falsafa ya jamii husika kwa kuwa vipengele vya falsafa ya Kiafrika vimejitokeza katika utenzi wa Nyakiiru Kibi. Vipengele hivyo ni pamoja na utendaji wa matambiko na kafara, imani kuhusu ulimwengu wenye nyuga tatu, imani kuhusu uganga na uchawi, familia pana ya Kiafrika, kuthamini uzazi, ubuntu na ujumi wa Mwafrika.