Uchangamani wa Muundo wa Majina ya Watu: Mifano kutoka Lugha ya Kihaya

Authors

  • Adventina Buberwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Abstract

Makala hii inaangazia muundo wa majina ya watu yanayotokana na lugha ya Kihaya. Mjadala kuhusu muundo wa majina hayo unaongozwa na madai kwamba majina ya pekee si nomino halisi (Coates, 2006). Makala hii inalishughulikia suala hili kwa mkabala wa kimofolojia ili kubainisha wazi muundo wa majina tajwa. Data ya makala hii ilikusanywa kwa njia ya usaili kutoka Wilaya ya Bukoba Vijijini, mkoani Kagera. Matokeo yanaonesha kwamba majina ya watu ni vipashio vyenye muundo changamani ambavyo vikirejelewa kama nomino kimofolojia husababisha mkanganyiko wa kidhana. Hoja hii inathibitishwa na miundo mbalimbali ya majina ya watu iliyobainishwa katika makala hii ambayo ni pamoja na majina yenye muundo wa kitenzi, muundo wa kivumishi, muundo ambatani, muundo wa kishazi kiulizi na muundo wa kishazi cha kusihi. Kwa ujumla, ni wazi kwamba si kila kinachotajwa kuwa nomino kisemantiki ni nomino kimofolojia. Hivyo, makala hii inatoa wito wa kuchunguza vipengele vya kiisimu kwa kuzingatia dhana zinazoendana na mkabala unaohusika ili kuepuka mkanganyiko.

http://doi.org/10.56279/jk.v85i1.11  

Author Biography

Adventina Buberwa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Mhadhiri mwandamizi

Published

2023-04-03

Issue

Section

Articles