Usawiri wa Unyanyasaji wa Kiuchumi dhidi ya Wanawake katika Riwaya ya Kiswahili

Authors

  • Ernesta S. Mosha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Abstract

Makala hii inajadili unyanyasaji wa kiuchumi kwa wanawake kama ulivyosawiriwa katika riwaya ya Kiswahili. Makala inatumia dhana ya vilongo zoeleka  katika unyanyasaji wa wanawake ili kuweka bayana namna unyanyasaji wa kiuchumi unavyochochewa na mambo kama vile ubabedume na mila na desturi. Data za makala hii zimekusanywa kutoka katika riwaya teule tatu za Kiswahili ambazo ziliteuliwa kutokana na kusawiri aina mbalimbali za unyanyasaji wa kiuchumi kwa wanawake. Makala inabainisha namna vilongo zoeleka katika unyanyasaji wa wanawake vilivyotumika kuonesha jinsi baadhi ya wanaume wanavyofanikisha azma yao ya kuwanyanyasa wanawake kiuchumi. Aidha, makala imebainisha jinsi kilongo cha mfumo wa kijamii na ujifunzaji kitabularasa kilivyotumiwa na waandishi kuonesha kuwa wanaume wanyanyasaji hawana makosa kwa kuwa hawakufanya unyanyasaji huo kwa makusudi. Makala inaweka wazi kuwa usawiri wa aina hii una athari ya kuchochea unyanyasaji wa kiuchumi dhidi ya wanawake na kuimarisha mtazamo kuwa unyanyasaji wa aina hii ni jambo la kawaida na haliwezi kuepukika. Kwa upande mwingine, kilongo cha ukombozi wa binadamu wa kiharakati kimetumiwa kuonesha wazi kuwa baaadhi ya wanaume wanawanyanyasa wanawake kiuchumi kwa makusudi kwa hiyo wanastahili kuwajibishwa kutokana na unyanyasaji huo. Kwa kuwa riwaya zina nafasi kubwa ya kutambulisha njia mbadala za kukabiliana na aina mbalimbali za unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kiuchumi, ni muhimu vilongo mbadala vikatumika katika riwaya ya Kiswahili ili kusaidia kubadili tabia za wanaume wanyanyasaji pamoja na mtazamo kuhusu unyanyasaji wa kiuchumi dhidi ya wanawake.

 http://doi.org/10.56279/jk.v85i1.13  

Author Biography

Ernesta S. Mosha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Mhadhiri mwandamizi

Published

2023-04-03

Issue

Section

Articles