Dhima ya Kialami Pragmatiki ' Hivi ' katika Mawasiliano ya Kiswahili
Abstract
Makala hii inahusu dhima za kialami pragmatiki hivi katika mawasiliano ya Kiswahili. Data za makala hii zimekusanywa kutoka katika mazungumzo yanayofanywa katika vijiwe vya mamalishe, vipindi vya televisheni na kutoka katika soga za mtandao wa WhatsApp. Uchambuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Umuktadhaishaji ya Gumperz (1982) na kwa kutumia mbinu ya uchambuzi kilongo. Matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kwamba kialami pragmatiki hivi kina dhima tofautitofauti kinapotumiwa katika mawasiliano. Miongoni mwa dhima hizo ni kutumika kama kianzilishi cha swali, kusisitiza jambo, kunukuu mazungumzo, kuashiria wakati uliopo au muda si mrefu, kudokeza makadirio au kutokuwa na hakika ya jambo na kutumika kama kiolezi. Kwa ujumla, makala hii inadokeza kwamba lugha ya Kiswahili ina utajiri wa kimaana unaotokana na matumizi ya vialami pragmatiki. Hivyo, tafiti zaidi zinaweza kufanyika kuchunguza dhima za vialami pragmatiki vingine katika lugha hii.