Faida ya Kujifunza kwa Kuegemea Mfumo wa Isimu ya Kiswahili: Mfano wa China

Ning Yi, Maiso Bosire

Abstract


Makala[1] hii inachunguza changamoto na faida zilizopo kwa wanaojifunza Kiswahili kwa kutumia mifumo ya kiada iliyopo nchini China. Mifumo hii inaweza kujumuishwa katika makundi mawili[2]. Kundi la kwanza ni mfumo ulioenea nchini China, kama maeneo mengine, ulimwenguni ambao hugawa nomino katika umoja na wingi kama kielelezo kikuu. Kundi la pili ni mfumo ambao umetungwa kwa kuiegemea isimu ya Kiswahili na ya lugha yake mame ya Kibantu. Data zilikusanywa uwandani kwa njia ya hojaji andishi na mahojiano ya ana kwa ana. Mbinu zilizotumika katika uchanganuzi wa data ni mkabala wa kimaelezo. Uchambuzi uliongozwa na Nadharia ya Uamilifu. Matokeo yanaonesha kuwa mfumo ulioenea China, si tofauti na ule ulioanzishwa nyakati za ukoloni, wakati ambapo mfumo wa isimu ya Kiswahili haukutambulika na hata manufaa yake katika utunzi wa mitaala na vitabu vya Kiswahili hayakutiliwa maanani. Ingawa hali hii huonekana kama inawafaa wanaoanza kujifunza Kiswahili angalau mwanzoni, baada ya muda mfupi huwa bayana kuwa baadhi ya masuala yanayofundishwa katika lugha hii hayaelezeki kwa njia mwanana kimfumo.

http://doi.org/10.56279/jk.v86i1.3

[1] Makala hii inatokana na wasilisho letu katika Kongamano la Kimataifa la Utafiti wa Lugha na Tamaduni za Afrika (International Conference on African Language and Culture Studies), Beijing, mwaka 2021. Katika wasilisho hilo, tulichunguza na tukaeleza tofauti za kiada katika kujifunza Kiswahili, hasa vyuoni, kwa kuangazia hali ilivyo kwetu katika Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) na hatimaye tukabaini faida za kutumia mfumo wa kuzingatia isimu ya Kiswahili kama kielelezo kikuu.

[2] Ingawa tunataja makundi mawili, baadaye tutayaweka pamoja na kuijadili kama mifumo miwili. Hii ni kwa sababu, ndani ya kila kundi, dhana kuu iliyo msingi wa mfumo ni ileile. 


Full Text:

 Subscribers Only

Refbacks

  • There are currently no refbacks.