Uathirianomatini wa Kimtindo katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa "Utenzi wa Hati" na "Utenzi wa Mwanakupona"

Authors

  • Ali H. Chembea Islamic University
  • Furaha J. Chai Chuo Kikuu cha Pwani
  • Rocha M. Chimerah Chuo Kikuu cha Pwani

Abstract

Bakhtin (1981) anaeleza kwamba matini za kifasihi huathiriana na kuhusiana. Kila matini ya kifasihi ina sauti zinazoingiliana na kuhusiana na matini nyingine zilizopo, zilizopita au zijazo. Hata hivyo, Bakhtin haoni kama ushairi una uathiriano na ushairi mwingine sawia kama inavyojitokeza katika riwaya. Baadhi ya wataalamu waliohakiki "Utenzi wa Hati" na "Utenzi wa Mwanakupona" wamedai kuwa tenzi hizi zimeathiriana. Makala hii inalenga kudhihirisha uathirianomatini wa kimtindo kati ya "Utenzi wa Hati" na "Utenzi wa Mwanakupona" katika ushairi wa Kiswahili. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Usemezano ya Bakhtin. Ingawa kwa mujibu wa nadharia hiyo, riwaya ndio utanzu unaotegemea zaidi uathiriano na matini nyingine kuliko ushairi, makala hii inapanua mawanda yake kwa kuchunguza uathiriano wa kimtindo katika ushairi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwapo kwa uathiriano wa muundo, msamiati, majibizano na tamathali za semi.

http://doi.org/10.56279/jk.v86i1.5

Published

2024-01-16

Issue

Section

Articles