Iktibasi katika Methali za Waswahili
Abstract
Makala hii inalenga kuchunguza namna iktibasi inavyojitokeza katika methali za Waswahili. Iktibasi ni dhana ya Kiarabu kwa mujibu wa Karisa na Mwinyifaki (2013). Ni mbinu ya kuchota mafundisho ya Kurani Tukufu na Sunnah na kuyatumia katika fasihi bila kuonesha yametoka katika Kurani Tukufu na Sunnah (Karisa na Mwinyifaki, 2013). Maisha ya Waswahili licha ya kuongozwa na maadili yaliyomo katika mafundisho ya dini ya Kiislamu, methali zinazotumiwa na Waswahili hao katika mazungumzo yao ya kila siku pia huchangia kutilia nguvu mafundisho ya dini. Uchunguzi huu umechochewa na methali za jamii ya Waswahili ambazo zinaelekea kusheheni mafundisho ya dini. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uislamu kwa mujibu wa mawazo ya Hashi (2011) katika kubainisha namna mafundisho ya Kurani na Hadith yanavyojitokeza katika methali za Waswahili. Matokeo ya utafiti yalionesha kwamba methali za Waswahili zilisheheni mafundisho ya maadili ambayo yalipatikana pia katika Kurani na Hadith. Uhusiano mwema kati ya binadamu na binadamu na binadamu na Mungu unapatikana katika methali, na Kurani na Hadith vilevile.a