Riwaya za Euphrase Kezilahabi kama Nyenzo Mwafaka za Ukuzaji wa Stadi ya Tafakuri Tunduizi: Mfano wa Nagona na Mzingile

Authors

  • Wallace Kapele Mlaga na Laurien Tuyishim University of Dar es Salaam

Abstract

 

Lengo kuu la makala hii ni kujadili namna riwaya za Euphrase Kezilahabi zinavyoweza kutumiwa kama nyenzo ya kukuza stadi ya tafakuri tunduizi. Ili kufanikisha lengo hili, makala imeshughulikia malengo mahususi mawili: kwanza, makala inajadili namna stadi ya tafakuri tunduizi inavyosawiriwa katika riwaya teule za Kezilahabi na hivyo kuzifanya riwaya husika kuwa nyenzo mwafaka za ukuzaji wa tafakuri tunduizi. Pili, kubainisha namna riwaya teule zinavyosawiri umuhimu wa stadi ya tafakuri tunduizi. Ili kufanikisha malengo haya, data zilikusanywa kupitia mbinu ya uchambuzi wa matini. Data hizi zilichambuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Uhalisia na Nadharia ya Semiotiki. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba riwaya za Nagona na Mzingile ni nyenzo mwafaka za kukuza tafakuri tunduizi kwa sababu riwaya hizi zinasawiri matendo mbalimbali yanayofanywa na wahusika kutokana na kutokuwa na stadi ya tafakuri tunduizi: kuyumbayumba kiimani kwa waumini na watu kutotatua changamoto zinazowakabili na badala yake kupendelea kumuachia Mungu. Aidha, umuhimu wa tafakuri tunduizi umesawiriwa katika riwaya teule. Tafakuri tunduizi imeonekana kuwa na umuhimu ufuatao: kuwezesha ufanyaji wa maamuzi sahihi na kusaidia kutengeneza maarifa mapya. Makala inahitimisha kuwa riwaya teule ni nyenzo mwafaka za ukuzaji wa tafakuri tunduizi kwa kuwa zinaonesha sio tu madhara ya kutokuwa na tafakuri tunduizi bali pia umuhimu wake.

   

http://doi.org/10.56279/jk.v86i2.4

Published

2024-04-09

Issue

Section

Articles