RUWAZA ZA KIMOFOLOJIA ZA MAJINA YA MAHALI YA KIHAYA: MTAZAMO WA MOFOLOJIA LEKSIKA

Authors

  • Adventina Buberwa

Abstract

Makala haya yamechunguza ruwaza za majina ya mahali ya Kihaya 9 kwa kuchanganua vijenzi
mbalimbali vinavyojenga majina hayo. Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa
kutoka katika wilaya za Muleba, Missenyi, Bukoba Vijijini na Bukoba Mjini, mkoani Kagera kwa
ajili ya tasnifu ya Uzamivu. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika
kwa mujibu wa Kiparsky (1982) inayosisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno vimepangwa
kidarajia kimsonge ambapo vipashio vidogo huungana ili kuunda vipashio vikubwa. Data za
utafiti huu zimewasilishwa kwa kutumia majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwa
kwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika na
kuonesha jinsi vipashio hivyo vilivyopangwa kidarajia kimsonge. Matokeo ya uchanganuzi huo
yamedhihirisha kuwa majina ya mahali yaliyochunguzwa yameundwa kwa vijenzi mbalimbali
ambavyo vimechanganuliwa kimofolojia. Tofauti na madai ya baadhi ya wanaisimu kuwa majina
ya mahali yameundwa na mizizi au mashina tu, makala haya yamethibisha kuwa vipo vipashio
maalumu vinavyounda majina ya mahali na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia.

Downloads

Published

2017-05-25

Issue

Section

Articles