Tathmini ya Hatua za Tafsiri kama Nyenzo ya Ufanisi wa Mawasilino

Authors

  • Hadija Jilala University of Dar es salaam

Abstract

Makala haya yanahusu tathmini ya hatua za tafsiri kama nyenzo ya ufanisi wa mawasiliano. Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uzalishaji wa tafsiri bora na sadifu yenye ushikamani wa maana na ujumbe wa matini chanzi katika matini lengwa. Makala haya yanajadili kwamba, endapo mfasiri hatafuata hatua thabiti za tafsiri anaweza kuzalisha tafsiri iliyokengeuka katika maana na ujumbe. Kwa hiyo, lengo la makala haya ni kupima utendekaji wa hatua za tafsiri zilizopendekezwa na Jilala (2014) katika modeli yake ya MMK1 ili kuonesha namna hatua hizo zinavyoweza kutumika katika muktadha halisi wa zoezi la mchakato wa tafsiri. Katika kujadili jinsi hatua hizo zinavyotumika kutafsiri matini za kitamaduni, makala haya yanapima ufaavu wa hatua hizo kama mwongozo wa kutafsiri matini za aina zingine. Makala haya yanajadili kuwa hatua hizo zinaweza kutumika kama mwongozo wa kutafsiri matini za aina nyingine na ni nyenzo madhubuti ya kufikia ufanisi wa mawasiliano kwa jamii za lugha tofauti.Tafsiri yoyote haiwezi kuwa sadifu kama mfasiri hatazingatia hatua muafaka za kutafsiri. Kwa maana hiyo, hatua za tafsiri ni kipengele muhimu katika kuwasilisha maana na ujumbe sadifu wa matini chanzi katika matini lengwa ili kufanikisha mawasiliano.

1 Modeli ya Mawasiliano ya Kitamaduni ambayo ilipendekezwa na Jilala (2014) kama mwongozo wa kinadharia wa kutafsiri matini za kitamaduni. Katika modeli hii, hatua za tafsiri ni moja ya kijenzi cha modeli ambazo zilipendekezwa kama hatua za kutafsiri matini za kitamaduni baada ya data za utafiti kudhihirisha kuwa hatua zilizopendekezwa an Newmark (1988) na baadaye Mwansoko (1996) kujikita katika ujumla na kuonekana zinakwama katika kutafsiri matini za kitamaduni.

Author Biography

Hadija Jilala, University of Dar es salaam

Mwalimu katika Taasisi ya Kiswahili (Chuo Kikuu Cha Dar es salaam)

Downloads

Published

2016-02-15

Issue

Section

Articles