Ufinyaji wa Fursa za Kiswahili Nchini Tanzania

Uchunguzi Kifani wa Sera ya Lugha na Mpangolugha

Authors

  • Elishafati J. Ndumiwe Chuo Kikuu cha Mt. Agustino cha Tanzania (SAUT) - Mwanza

Abstract

Mpangolugha nchini Tanzania huipa lugha ya Kiingereza hadhi ya juu, Kiswahili hadhi ya kati na lugha za kijamii hadhi ya chini (Msanjila, 2009; Rugemalira, 2013; Ndumiwe, 2019; Kawonga, 2023). Lugha iliyopewa hadhi ya juu hutumika katika shughuli rasmi kama vile mahakama za juu, diplomasia, mikataba na shughuli za kimataifa. Fursa katika lugha hutegemea mawanda mapana ya matumizi ya lugha inayobidhaishwa. Hata hivyo, lugha ya Kiswahili nchini Tanzania imepewa mawanda finyu katika shughuli rasmi ikilinganishwa na lugha ya Kiingereza. Kwa hiyo, utafiti huu unachunguza namna mpangolugha na sera ya lugha vinavyofinya fursa za  Kiswahili nchini Tanzania. Data za makala hii zimekusanywa maktabani na uwandani. Kwa upande wa maktabani, data zilikusanywa kutoka andiko la Sera ya Utamaduni (WEU, 1997) kwa kutumia mbinu ya usomaji wa matini. Aidha, kwa upande wa uwandani, data zilikusanywa kutoka kwa wahitimu wa ualimu katika Kiswahili, wafasiri, wakalimani na walimu wa shule za sekondari kwa kutumia mbinu ya usaili. Nadharia ya Ikolojia ya Kiisimu iliyoasisiwa na Wendel (2005) ilitumika katika kuchanganua data za utafiti huu. Utafiti huu umebaini kuwa mpangolugha na sera ya lugha huminya fursa katika Kiswahili kama vile tafsiri, ukalimani, ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni, uhariri na uchapishaji katika Kiswahili. Utafiti huu unapendekeza kuandaliwa kwa sera ya lugha na mpangolugha mpya ili kuiweka lugha ya Kiswahili katika darajia la juu. Suala hilo litaongeza fursa za kiuchumi katika lugha ya Kiswahili.

 

http://doi.org/10.56279/jk.v87i2.3

Published

2024-12-31