HADHI YA KISWAHILI NA WATUMIAJI WAKE KATIKA UTANDAWAZI

DeoGratias K Tungaraza

Abstract


Kwa mujibu wa wanazuoni, Nurse na Spear (1985:1) Kiswahili kimeanza kuzungumzwa tangu mapema katika milenia ya kwanza toka kuzaliwa Kristo, yaani mnamo miaka ya 800 hadi 1000. Tangu wakati huo Kiswahili kimekuwa sumaku ya kuwavuta pamoja, kuwaunganisha na kujenga uhusiano madhubuti miongoni mwa wasemaji wa lugha hii, wa makabila na/au mataifa anuwai. Ama kwa hakika, hapana mahali ambapo hali hiyo ni dhahiri kabisa Barani Afrika, au kwingineko duniani, kama katika janibu yetu hii ya Afrika ya Mashariki. Katika Taifa la Tanzania, mathalani, Kiswahili kimewakusanya na kuwajumuisha pamoja watu wa makabila zaidi ya 150 – kikitumika kama lugha ya mawasiliano inayoeleweka na watu wote.  Hii si ajabu, ikizingatiwa kuwa, kwa silika yake, Kiswahili ni lugha unganishi, yaani yenye hulka ya kuunganisha, na siyo ya kutenganisha au ya kibaguzi (Mazrui & Mazrui 1999) kama, kwa mfano, Kiafrikaans. Aidha, katika harakati za mapambano ya kuleta uhuru, na, hatimaye, Muungano, Kiswahili ndicho kilikuwa mkuki wa kuwachomea na kuwafukuzia mbali Wakoloni; na ngao madhubuti ya kudhibiti Wakoloni dhidi ya mbinu ambazo zilikuwa hasidi na zenye ulaghai mwingi zilizotumia mbinu ya ‘tenganisha utawale.’ Kutokana na uthabiti wa Kiswahili, mbinu hizo hazikufua dafu! Na wakoloni walipotahamaki TAA kuwa imekwishazaa TANU, kiboko chao; na kule Visiwani, kuwa ASP imekwishatwaa nchi!

 


Full Text:

pdf

Refbacks

  • There are currently no refbacks.