MATUMIZI YA MKABALA WA KIBWEGE KATIKA UCHAMBUZI WA TAMTHILIA YA AMEZIDI (1995) YA S. A. MOHAMED

Authors

  • Zawadi Limbe Daniel

Abstract

Mkabala wa Kibwege katika uandishi wa kazi za fasihi unasemekana kuibuka baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Kuibuka kwake kunahusishwa na ugumu wa maisha uliowakabili watu baada ya vita hivyo, ambapo ugumu huo uliwafanya watu kuyaona maisha kuwa hayana maana. Katika kazi za fasihi zenye sifa ya mkabala huu, kaida, taratibu na kanuni za utunzi zinakengeushwa.   Katika fasihi ya Kiswahili, mkabala huu unajitokeza sana katika tamthilia ya Amezidi (1995), kwani tamthilia hii haifuati ruwaza na kanuni za utunzi wa tamthilia zilizozoeleka. Makala haya yanakusudia kuchambua, kuainisha na kuhakiki matumizi ya vipengele mbalimbali vya mkabala wa Kibwege katika tamthilia ya Amezidi. Makala yatahakiki pia muktadha na chanzo cha kuibuka kwa kazi za kibwege katika Afrika Mashariki ikilinganishwa na mkabala uliozalisha fasihi hiyo kule Ulaya baada ya Vita vya Pili.

 

Downloads

Published

2017-08-11

Issue

Section

Articles