Usawiri wa Falsafa ya Uduara kama Nyenzo ya Kutafsiri Maisha ya Mwafrika katika Riwaya za Nagona na Babu Alipofufuka
Abstract
Makala hii inalenga kubainisha kwamba uduara ni nyenzo muhimu ya kutafsiri maisha ya Mwafrika katika nyanja mbalimbali. Uduara ni dhana ya kifalsafa inayobainisha kuwa maisha ni mzunguko unaojirudia. Utafiti wa makala hii ulifanyika maktabani. Mbinu ya uchambuzi wa matini na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika vimetumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo yanaonesha kuwa dhana ya uduara ina uwezo mpana wa kufasili maisha ya Mwafrika, ikijikita katika muktadha wa kiroho, muktadha wa urithishaji wa maarifa, pamoja na muktadha wa kiujumi. Makala inahitimisha kuwa falsafa ya uduara inapaswa kuchukuliwa kama dira ya kuongoza maisha, maadili na maarifa ya Mwafrika katika nyanja zote za maisha.
Downloads
Published
2025-06-30
Issue
Section
Articles