Mchango wa Washirazi katika Historia ya Lugha na Utamaduni wa Waswahili

Authors

  • Mussa M. Hans Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Kwa muda mrefu, kumekuwa na mjadala endelevu kuhusu historia ya lugha ya Kiswahili, hususani katika kipengele cha utamaduni wa Waswahili na jamii ya Waswahili kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa, utamaduni wa Waswahili katika upwa wa Afrika Mashariki umekuwa ukihusishwa na ujio wa Waarabu. Hata hivyo, mbali na Waarabu ambao wamekuwa wakihusishwa kwa karibu na lugha pamoja na utamaduni wa Waswahili, matokeo ya utafiti tulioufanya kisiwani Zanzibar yanaonesha kwamba Washirazi nao wana mchango katika historia ya lugha na utamaduni wa Waswahili kwa ujumla. Hivyo, lengo la makala hii ni kujadili mchango wa Washirazi katika historia ya lugha na utamaduni wa Waswahili. Mjadala katika makala hii unaongozwa na Nadharia ya Mwachano na Makutano ya Lugha za Kibantu iliyoasisiwa na Massamba (2007). Makala hii ni matokeo ya utafiti wa maktabani na uwandani uliofanyika katika maeneo ya Unguja na Pemba. Data za uwandani zimefafanuliwa kwa kuhusishwa na maandiko mbalimbali kuhusu jamii zilizohusishwa katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti uliozaa makala hii yanaonesha kwamba Washirazi wana mchango mkubwa katika maisha na historia ya jamii ya Waswahili ingawa hawatajwi sana katika kazi nyingi zinazohusu historia ya Kiswahili. Neno Kiswahili katika makala hii linachukuliwa kwa maana ya lugha na utamaduni wa wazungumzaji wa lugha hiyo.

http://doi.org/10.56279/jk.v88i1.8

Published

2025-06-30

Issue

Section

Articles