Uchunguzi wa Ikolojia-Ubeberu katika Fasihi ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Nakuruto ya Clara Momanyi

Authors

  • Lina Akaka Chuo Kikuu cha Daystar

Abstract

Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, fasihi ya Kiswahili imekuwa ikitoa mchango mkubwa kuhusu masuala ya mazingira kupitia tanzu mbalimbali za fasihi andishi na fasihi simulizi. Miongoni mwa kazi za kwanzakwanza kushughulikia suala la mazingira katika fasihi ya Kiswahili nchini Kenya ni riwaya ya Nakuruto (2009) ya Clara Momanyi. Riwaya ya Nakuruto ilitungwa wakati ambapo kazi za fasihi ya kimazingira zilikuwa haba. Makala hii inalenga kuchunguza jinsi riwaya hii inavyokosoa ubeberu dhidi ya mazingira uliofanywa na wakoloni na wenyeji. Shughuli za unyonyaji wa rasilimali za wenyeji kwa manufaa ya Wamagharibi na wenyeji zimechunguzwa pia. Riwaya ya Nakuruto iliteuliwa kimakusudi ili kuchunguza suala la ikolojia-ubeberu. Mbinu ya ukusanyaji data ya usomaji makini wa riwaya teule ilitumiwa, data ilinakiliwa na kutiwa katika mada ndogondogo. Mtafiti alinukuu madondoo yanayolenga suala la ikolojia-ubeberu katika riwaya, akayafasiri na kunukuu wanayoyasema wasomi wengine kuhusu suala hilo huku akiongozwa na Nadharia ya Uhakiki-ikolojia. Matokeo ya utafiti yalionesha bayana kwamba binadamu huyatawala na kuyaharibu mazingira kiasi cha kuhatarisha uhai katika sayari. Mwanadamu amekuwa akinyonya maliasili na kuonesha sifa za ubeberu zilizojaa choyo, ubinafsi na tamaa katika harakati yake ya kujinufaisha kutokana na maliasili ambayo inajumlisha vyanzo vya maji, milima, udongo, madini pamoja na miti.

http://doi.org/10.56279/jk.v88i2.1

Downloads

Published

2025-09-02

Issue

Section

Articles