Miti kama Elementi ya Udhibiti wa Miundomsingi ya Kijani katika Diwani Teule za Ushairi wa Kiswahili

Authors

  • Mwaniki Mugwe Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Rayya Timammy Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Omboga Zaja Chuo Kikuu cha Nairobi

Abstract

Makala hii inalenga kubainisha uanuwai wa miti kama miongoni mwa elementi asilia na ya msingi katika udhibiti wa miundomsingi ya kijani katika diwani teule za ushairi wa Kiswahili. Tumeteua diwani za ushairi za Kina cha Maisha (Mohammed, 1984), Jicho laNdani (Mohammed, 2002), Msimu wa Tisa (Mberia, 2007) na Doa (Mberia, 2018) kama vyanzo vya data yamsingi. Ili kutimiza lengo hili, tumetumia mbinu ya usampulishaji lengwa katika kuteua kazi zilizotoa data ambazo tumezichambua kwa kutumia njia ya maelezo. Fauka ya haya, tumeongozwa na Nadharia ya Fasihi Ikolojia ambayo kimsingi inaangazia uhusiano na mwingiliano baina ya binadamu na mazingira anamoishi(Glotfelty, 1996). Matokeo yanaonesha kuwa utunzajina uhifadhi wa miti ni miongoni mwa elementi ya miundomsingiya kijani ambayo hudhibiti na kufanikisha uendelevu wa mfumo tata na changamani wa uhaianuwai. Mathalani, kupitia miti, binadamu anapata afya njema, dawa na tiba za jadi na za kisasa na uimarikaji wa uchumi kutokana na rasilimali zinazozalishwa kutokana na miti. Vilevile, miti inatumika katika udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi, hifadhi ya baadhi ya spishi zawanyamapori kama vile mijusi na nyani.

http://doi.org/10.56279/jk.v88i2.2

Downloads

Published

2025-09-02

Issue

Section

Articles