Nyimbo Shambulizi za Bongo Fleva katika Siasa Liberali Tanzania

Authors

  • Fokas Nchimbi Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa, Tanzania Anuani ya Barua Pepe: fokasnchimbi@gmail.com

Abstract

Kizazi cha pili cha siasa za Afrika kimeshuhudia kuingia kwa   siasa liberali (liberal politics) zilizotokana na mashinikizo ya siasa za kimataifa za Magharibi kama vile masharti kwa nchi za Kiafrika kupatiwa misaada kufuatia hali ngumu za kijamii na kiuchumi kwa upande mmoja. Kwa upande mwingine pamekuwapo na sababu za ndani za misukumo ya kuingiza na kuendesha siasa liberali katika nchi ya Tanzania na nchi nyingine za mataifa ya Kiafrika. Makala hii inaeleza maudhui ya nyimbo shambulizi katika zama za uliberali katika nchi ya Tanzania kuanzia mapema miaka ya tisini. Inaeleza kuwa katika Tanzania, kama ilivyokuwa kwa nchi nyingi za Kiafrika, nyimbo shambulizi- zilizoushambulia ukoloni mkongwe, ukoloni mamboleo, na siasa za kibepari- zilianza kufifia baada ya nchi kupata uhuru mwaka 1961 na baada ya kuingia kwenye siasa za chama kimoja mwaka 1965. Katika utawala wa serikali ya chama kimoja (1965 €“ 1992) mwelekeo wa nyimbo nyingi ulikuwa ni kusifu viongozi wa taifa na kuhamasisha sera zao bila kujali kama zilikuwa ni sahihi na kama   zingeweza kutekelezeka au la. Haikuwa rahisi kwa wasanii kwenye tasnia ya muziki kutunga na kuimba nyimbo za kuwashambulia viongozi wa siasa katika Tanzania kwa sababu ya kuwapo kwa udhibiti mkali wa kisiasa dhidi ya ukosoaji wa aina yoyote. Kwa kutumia mkabala wa Umaksi   makala hii inaonesha kuwa baada ya kuingia kwa mfumo wa siasa za kiliberali kumezuka   wimbi la nyimbo shambulizi nyingi zenye dhima ya kulaumu, kukosoa, na kupinga mifumo ya kifisadi na utendaji mbaya wa viongozi na watendaji katika taasisi   za serikali na mashirika ya umma nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali. Wanamuziki wa kizazi kipya   (Bongo Fleva) wametunga kazi nyingi za   kuwaponda wanasiasa   na sera zao kama vile katika nyimbo ' Ndio Mzee ' (Profesa Jay)   na ' Deni la Hisani ' - ' A Debt of Courtesy ' (Mrisho Mpoto). Makala hii inaonesha maeneo yanayolalamikiwa na makundi ya watu wanaotetewa kama makundi ya   tabaka la watawaliwa katika mashambulizi yao

Author Biography

Fokas Nchimbi, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa, Tanzania Anuani ya Barua Pepe: fokasnchimbi@gmail.com

Mwalimu

Downloads

Published

2018-05-09

Issue

Section

Articles