Kiswahili na Ukombozi wa Jamii

Authors

  • Kiarie Wa'njogu Chuo Kikuu cha Yale (Marekani) John.wanjogu@yale.edu

Abstract

Mawasiliano ni muhimu katika utekelezaji wa malengo yoyote yale yanayohusisha kikundi cha watu wawe ni wa shirika, kabila, eneo, au nchi fulani. Kama chombo cha mawasiliano, lugha imekuwa ikitumika kupashana habari katika nyanja mbalimbali. Kwa muda mrefu, binadamu ametambua umuhimu wa lugha katika kuunganisha na kutenganisha watu (pale inapolazimu), kusuluhisha matatizo kunapotokea kutoelewana, na kuborasha maisha kwa jumla.   Mbinu ya kutenganisha watu kwa misingi ya lugha ilitumiwa sana katika enzi za wakoloni kudhoofisha watu wa nchi moja, lakini wa makabila mbalimbali, ili jitihada zao za kujikomboa zisifue dafu (Gjersø, 2015).   Kwa sababu hii, watu wa kabila moja (wasemi wa lugha moja) walizuiliwa kutangamana na watu wa makabila mengine na ikilazimika kufanya hivyo walihitajika kupata kibali maalumu cha kuwawezesha kusafiri kutoka "eneo" lao hadi lingine.   La ajabu ni kwamba hata baada ya nchi nyingi kurudishiwa uhuru wao na kuweko kwa uhuru wa kutangamana, mbinu hii ya kutenganisha watu bado imeendelea kufuatwa (kwa kujua au kutojua) kwa kuzingatia sera ambazo zinaweza kufasiriwa kuwa vizuizi, kwa njia moja au nyingine, vya ukombozi wa kiuchumi, kisiasa, na kijamii.   Katika makala hii, tutachunguza ni kwa kiasi gani lugha ya Kiswahili imefaulu na ni wapi imefeli katika kuhitimisha lengo la ukombozi katika nyanja muhimu za maisha ya watumiaji wa lugha hii. Tutachunguza nini hasa kimechangia katika kufaulu/na kufeli huku.   Tutahitimisha kwa kupendekeza namna ya kukihusisha Kiswahili zaidi kama chombo cha ukombozi wa eneo linalotumia lugha hii

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biography

Kiarie Wa'njogu, Chuo Kikuu cha Yale (Marekani) John.wanjogu@yale.edu

Mwalimu

Downloads

Published

2018-05-09

Issue

Section

Articles