Mitindo ya Lugha Ibuka katika Mitandao ya Kijamii: Mifano kutoka Mawasiliano ya Facebook

Toboso Mahero Bernard, Mosol Kandagor, Allan Opijah

Abstract


Matumizi ya teknolojia mpya yamesababisha kuzuka kwa mitindo mipya ya mawasiliano. Matumizi ya mitindo hii yalishika kasi baada ya kuvumbuliwa kwa mitandao ya kijamii kama ule wa Facebook uliovumbuliwa mwaka wa 2004. Kabla ya kuvumbuliwa kwa mitandao ya kijamii, mitandao iliyokuwepo haikuwapa watumizi wa intaneti mazingira yenye kunawirisha mitindo ya kimawasiliano kama yale yanayotolewa na vyombo vya habari vya kijamii kama Facebook. Mazingira yaliyotolewa na mitandao ya kijamii ni kama uhuru wa matumizi ya lugha, sera ya vipimo vya idadi ya herufi za kutumia katika mawasiliano, ujenzi wa makundi ya gumzo na familia za mtandaoni, uhuru wa ubunifu na uhuru wa watu kujichapishia ujumbe katika tarakilishi na rununu. Mazingira mengine ni gharama ya mawasiliano kutokana na kulipia kila ujumbe, uhuru wa uteuzi wa maudhui ya mawasiliano, kukubaliwa kwa lugha zote za ulimwengu kama lugha za mawasiliano ya mitandao na uwezo wa mitandao anuwai ya kijamii kufika pembe zote za ulimwenguni. Mazingira haya yamechangia katika chimbuko na usambaaji wa haraka wa mitindo mipya ya lugha ya kidijitali. Makala haya yanachunguza mitindo ya lugha ya kidijitali inayotumiwa katika mawasiliano ya Facebook.

 

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.