Fasihi katika Lahaja Ibukizi. Mifano kutoka Chapisho la "Shujaaz"

Authors

  • Pamela Ngugi Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya Barua Pepe: muhadiap@yahoo.com

Abstract

Katika miaka ya hivi karibuni, kumezuka mjadala kuhusu uwezekano wa kuchapisha vitabu na makala kwa kutumia msimbo wa Sheng. Kwa upande mmoja, kuna wale wanaodai kuwa Sheng ni msimbo unaowatambulisha vijana na hivyo basi msimbo huu unaweza kutumiwa ili kuwafikia vijana hawa kwa kuchapisha vitabu au hata makala mbalimbali yanayoweza kuwafaidi (Mugubi, 2006). Kutokana na mwelekeo huu, pameibuka kijitabu kwa jina "Shujaaz", ambacho hulenga vijana katika umri wa miaka mbalimbali. Makala hii inalenga kubaini uamilifu wa kijitabu cha Shujaaz ambacho hutumia lugha ya Sheng katika kuwasilisha jumbe mbalimbali kwa vijana. Mjadala huu utajikita katika muktadha wa taaluma ya fasihi, hasa ikichukuliwa kuwa fasihi huelemisha na huburudisha.   Tunalenga kuonyesha ni kwa namna gani, kupitia msimbo wa Sheng, masuala mbalimbali yanayohusu maisha ya vijana hujadiliwa. Makala itajadili maudhui mbalimbali yanayojadiliwa katika Shujaaz na kisha kuyaoanisha na taaluma nzima ya fasihi

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biography

Pamela Ngugi, Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya Barua Pepe: muhadiap@yahoo.com

Mwalimu

Downloads

Published

2018-05-09

Issue

Section

Articles