Ufutuhi katika Jamii za Watanzania: Mjadala kuhusu Sura za Utokeaji na Dhima zake

A. S. Ponera

Abstract


Makala haya yanafafanua jinsi ufutuhi unavyojitokeza kwa jamii ya Watanzania pamoja na dhima zake. Ufutuhi unajadiliwa humu kama hali za uchangamfu, furaha, na kicheko inayojengwa na maneno, matendo, matukio au mazingira yoyote yenye mnato na mvuto. Sura za utokeaji wa ufutuhi zinaoneshwa kupitia data 23 za ujumbe za kifutuhi zilizokusanywa kutoka katika vyanzo anuwai vya mifumo ya kimawasiliano itokanayo na maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hususani kupitia ujumbe wa kawaida, WhatsApp, facebook na baruapepe. Makala yanafafanua kuwa ufutuhi kwa jamii ya Watanzania hujitokeza katika sura za ufyosi, kejeli, dhihaka na vijembe. Sura hizo za utokeaji zimehusishwa na misingi ya nadharia tatu zinazoelezea utokeaji wa ufutuhi (Nadharia ya Mkwezo, Nadharia ya Msigano na Nadharia ya Burudiko). Kuhusu dhima, makala haya yanafafanua dhima kubwa nne za ufutuhi. Nazo ni: kuwa kiungo cha kijamii, kutekeleza sanaa au fasihi ya jamii husika, kielelezo cha ujumi, na kilainishi cha maisha ya sasa.

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.