Fasihi Tafsiriwa za Kigeni: Urafiki au Uadui kwa Fasihi ya Kiswahili

Authors

  • Joseph N. Maitaria University of Dar es salaam
  • Peter M. Kinyanjui
  • Leah Mwangi

Abstract

Makala haya yanafafanua mustakabali wa fasihi tafsiriwa za kigeni kwa fasihi ya Kiswahili. Kupitia tafsiri, fasihi hizo za kigeni zimekuwapo Afrika Mashariki wakati wa ukoloni na hata baada ya ukoloni. Katika enzi ya ukoloni na hasa katika miaka ya 1930, uhaba wa vitabu vya kufundishia Kiswahili na fasihi yake ulijitokeza. Vitabu hivyo vilihitajika kwa dharura ili kuitikia wito wa serikali ya ukoloni ya wakati huo. Kutokana na sera ya serikali ya ukoloni kuhusu lugha, kuliundwa Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki (ILC). Vitabu vichache vya lugha na fasihi vilikuwapo. Watunzi wachache wenyeji pia walijitokeza kuchangia wito huo. Harakati za kutafsiri kazi za fasihi za kigeni nazo ziliendelea hata baada ya mataifa hayo ya Afrika Mashariki kupata uhuru. Swali hapa ni: Kuna haja ya kuendelea kutafsiri fasihi za kigeni kwa Kiswahili? Fasihi tafsiriwa hizo za kigeni zina athari gani kwa fasihi ya Kiswahili? Katika muktadha huu, makala haya yanatathmini nafasi ya fasihi hizo na athari yake kwa fasihi ya Kiswahili. Kadhalika, makala haya yanapendekeza namna fasihi tafsiriwa za kigeni zinavyoweza kuichangia fasihi ya Kiswahili katika uwasilishaji na uhifadhi wa utamaduni wa wenyeji wa Afrika Mashairiki.

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biographies

Joseph N. Maitaria, University of Dar es salaam

Mwalim

Peter M. Kinyanjui

Mwalim

Leah Mwangi

Mwalim

Downloads

Published

2024-04-01

Issue

Section

Articles