U-Nigeria: Athari zake katika Filamu za Kiswahili nchini Tanzania
Abstract
Makala haya yanaangazia athari za U-Nigeria katika filamu za Kiswahili nchini Tanzania. Dhana hii ya U-Nigeria imetazamwa kama masuala yanayojadiliwa katika filamu za ki-Nigeria ambayo yamekuwa yakipatiwa nafasi ya kujadiliwa upya katika filamu za Kitanzania. Kupitia makala haya, filamu ya Kiswahili nchini Tanzania imeonekana inahitajika kuwa alama ya utambulisho wa utamaduni wa Kitanzania. Athari za U-Nigeria zimejadiliwa katika pande mbili: Athari za U-Nigeria kwa watayarishaji wa filamu za Kiswahili - Tanzania na athari za U-Nigeria kwa watazamaji wa filamu za Kiswahili -Tanzania. Tija na madhara ya U-Nigeria yamejadiliwa katika muktadha wa utayarishaji na utazamaji. Kwa kuhitimisha hili, imeonekana kuwa jamii inayoazima utamaduni wa jamii nyingine katika utambaji wa hadithi zake huiweka mbali sanaa na jamii husika. Hivyo, watayarishaji wa filamu za Kiswahili-Tanzania wanahitajika kutayarisha filamu ambazo zitakuwa sehemu ya tajiriba, silika, historia na maisha ya Kitanzania.Downloads
Download data is not yet available.