Mpaka kati ya Uganga na Uchawi: Uchunguzi kutoka Riwaya za Kiethnografia za Kiswahili

Authors

  • Lameck Mpalanzi University of Dar es salaam

Abstract

Uganga na uchawi ni kani za kiontolojia zilizojadiliwa na wataalamu wengi. Hata hivyo, baadhi ya wataalamu hao hawaoneshi mpaka wa kitaaluma kati ya uchawi na uganga, na nguvu nyingine za kimiujiza zenye athari. Pamoja na ukweli kuwa dhana hizi huenda sambamba katika mijadala mingi, uchunguzi wetu umebaini kuwa ipo haja ya kuzijazidili kipwekepweke kutokana na miujiza, mafumbo na sihiri zilizofumbatwa katika kila dhana. Hivyo, makala haya yanajenga hoja kuwa upo mpaka bayana kati ya mganga na mchawi kwa kuzingatia utendaji, dhima, viwango vya nguvu-hai, miiko wa fani hizo, nafasi ya ufantasia na uainishaji wa makundi ya fani hizo. Aidha, mifano kutoka riwaya za kiethnografia za Kiswahili zinabainisha kuwa uganga na uchawi ni fani zenye athari hasi na chanya kulingana na lengo, matumizi na ufungamani wake na jamii teule. Licha ya kuonesha mpaka wa fani hizi, zipo changamoto zinazonasibishwa na fani hizi. Changamoto hizi zinahusu vifo, masuala ya uzazi na magonjwa. Pia, fani hizi zinakabiliwa na umaskini, husuda, usaliti na kulipizana visasi. Vilevile, baadhi ya waganga na wachawi hujikuta wanyonge kisaikolojia na kukosa uhuru kwani wanawindwa na serikali za miji na vijiji.

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biography

Lameck Mpalanzi, University of Dar es salaam

Mwalim

Downloads

Published

2024-04-01

Issue

Section

Articles