Ufanisi wa Tafsiri za Viwandani Nchini Tanzania: Uchunguzi wa Vifungashio vya Dawa za Binadamu

Authors

  • Rehema Stephano Chuo Kikuu cha Dodoma
  • Fidel Dassan Gwajekera Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Makala haya yanahusu tafsiri za vifungashio vya dawa za binadamu. Lengo kuu la kuandika makala haya lilikuwa kuchunguza ufanisi wa tafsiri za vifungashio hivyo. Methodolojia ya utafiti huu imejumuisha upitiaji wa tafsiri na usaili kwa wafamasia na watumiaji wa dawa. Lengo la kuwasaili wafamasia ni kupata taarifa kuhusu dhima ya wamiliki wa viwanda vya dawa kufanya tafsiri. Usaili wa watumiaji wa dawa ulilenga kuangalia tija za tafsiri za vifungishio vya dawa, hasa katika Kiswahili kwa watumiaji hao. Matokeo ya utafiti wetu yanaonesha kuwa ufanisi wa tafsiri hufikiwa pale tafsiri inapokidhi dhima zake. Uchunguzi wa vifungashio vya dawa umeonesha matokeo ya aina mbili ambayo ni kufanikiwa na kutofanikiwa kwa tafsiri katika dhima zake. Kufanikiwa kwa tafsiri katika vifungashio vya dawa za binadamu kumejionesha katika dhima mbalimbali kama vile kufanikisha mawasiliano, kufundisha na kujifunza lugha, pamoja na kupanua soko na kuwapa amani walaji wa bidhaa. Kutofanikiwa kwa tafsiri hizi kumetokana na kasoro kama vile udondoshaji, upotoshaji wa taarifa muhimu na kutozingatia sarufi ya lugha lengwa. Kutokana na kutofanikiwa kwa tafsiri za vifungashio hivyo vya dawa, utafiti huu unapendekeza tafsiri sahihi kuzingatiwa ili kukidhi mawasiliano pamoja na dhima nyingine za tafsiri. Kwa kufanya hivyo, dawa zitaweza kununuliwa na watu wengi zaidi kutokana na kuelewa maelekezo yanayotolewa katika lugha mbalimbali.

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biography

Rehema Stephano, Chuo Kikuu cha Dodoma

Mwalim

Downloads

Published

2020-02-27

Issue

Section

Articles