Kiswahili kama Nyenzo ya Umoja na Mshikamano Nchini Kenya Ikilinganishwa na Nchini China

Authors

  • Miriam Osore Chuo Kikuu cha Kenyatta

Abstract

Mtaalamu mashuhuri wa Kiswahili, Shaaban Robert, anatukumbusha katika shairi lake kwamba "Titi la mama ni tamu hata la mbwa likiwa". Shairi hili mashuhuri linasisitiza hali ya kujivunia lugha yetu ya Kiswahili jinsi ambavyo mtoto mchanga anavyothamini titi la mama yake hata kama ni mtoto wa mbwa. Baada ya miaka zaidi ya 55, tangu uhuru tamko hili muhimu halijazingatiwa wala kuthaminiwa kwa dhati inavyohitajika. Maoni yetu ni kwamba Wachina wameweza kupata utaifa, uzalendo, utambulisho na maendeleo makubwa kwa kuyapa masuala ya lugha ya taifa kipaumbele. Makala haya yanachanganua suala la lugha nchini Kenya, kwa kulinganishwa na mfano wa sera ya lugha ya Uchina. Nchini Kenya Kiswahili kinazungumzwa kama lugha ya taifa na kimeenea kote nchini. Pia, Katiba ya Kenya ya 2010 ilikiteua kama lugha mojawapo rasmi nchini. Hata hivyo, hatujapiga hatua katika kuendeleza utaifa, uzalendo na utambulisho kupitia Kiswahili na kwamba kwa miaka mingi tumejaribu kuchukua hatua kadhaa za kuimarisha Kiswahili ambazo si thabiti. Kama Kichina, Kiswahili kina uwezo wa kuleta uzalendo, utaifa na utambulisho nchini Kenya. Kiswahili kina nafasi ya kukomesha ukabila na kuleta maendeleo makubwa nchini. Kwa hivyo, katika makala haya yanajaribu kuchanganua masuala ya kimsingi ya utambulisho, utamaduni na jitihada za kujipenyeza kwenye ulingo wa kimataifa na utandawazi. Historia ya sera ya lugha ya Uchina inatolewa kwa malengo ya kubainisha hatua zinazoweza kuchukuliwa na serikali ili kuimarisha utaifa, utambulisho na utangamano nchini Kenya.

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biography

Miriam Osore, Chuo Kikuu cha Kenyatta

Mwalim

Downloads

Published

2020-02-27

Issue

Section

Articles