Mchango wa Media za Video katika Ufundishaji wa Kiswahili kwa Wageni

Authors

  • Arnold B.G. Msigwa University of Dar es salaam

Abstract

Kujifunza lugha ya kigeni hasa katika kipindi ambacho mjifunzaji akiwa tayari anayo lugha ya kwanza, huambatana na matatizo mbalimbali. Sababu za matatizo haya, mbali na mambo mengine, yanasababishwa na tofauti za kiisimu baina ya lugha ya mjifunzaji na lugha anayojifunza. Pia, hutokana na tofauti za kiutamaduni na kimazingira. Hivyo, ni mchakato ambao wakati fulani hukatisha tamaa miongoni mwa wajifunzaji. Matumizi ya media anuwai vile video katika kufundishia lugha ndiyo suluhu ya matatizo. Kwa hiyo, makala haya yanabainisha mchango wa media za Video katika kufundishia lugha ya kigeni mahususi kwa ajili ya Kiswahili. Aidha, matokeo ya mahojiano yaliyofanywa mwaka 2018 kati ya mwandishi wa makala na wafundishaji wa Kiswahili kwa wageni katika kituo cha MS TCDC1 (MS Training Center for Development Cooperation) kuhusu matumizi ya video kwa wajifunzaji lugha ya Kiswahili, yanabainisha kuwa video huwasukuma wajifunzaji lugha ya Kiswahili kupenda kujifunza lugha hiyo. Vilevile, video inawapa hamasa (motisha) wajifunzaji wa lugha. Swali linaloibuliwa na makala haya ni: Je, media za kisasa kama vile video zinasaidiaje ujifunzaji wa Kiswahili ikiwa ni lugha ya kigeni?

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biography

Arnold B.G. Msigwa, University of Dar es salaam

mwalim

Downloads

Published

2020-02-27

Issue

Section

Articles