Sababu za Kuibuka, Kung’ara, na Kupotea kwa Wasanii katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva: Uchunguzi wa Kategoria Maalumu ya Nyimbo Hizo

Issaya Lupogo

Abstract


Muziki wa Bongo Fleva (BF) umekua kwa kiasi kikubwa sana nchini Tanzania. Muziki huo sasa umekuwa biashara tofauti na miaka ya 2000 ambapo wasanii waliishia kuwa maarufu tu bila kupata kipato kikubwa kama miaka ya hivi karibuni (miaka ya 2015 hadi sasa). Jambo la kushangaza na ambalo limemakinikiwa katika makala haya ni kwamba wasanii wengi wa Bongo Fleva huibuka na kung’ara zaidi kwa muda fulani katika muziki lakini baadaye hupotea katika tasnia hii. Kwa hivyo, makala haya yanaangazia sababu za wasanii hao kuibuka, kung’ara, na kupotea. Matokeo ya makala haya yametokana na tajriba ya mwandishi kwa kuwa yeye ni mdau mkubwa wa masuala ya muziki. Mwandishi ni msanii1 wa muziki wa BF kwa kiasi fulani na amekuwa akishiriki katika kipindi cha redio2 ambacho pamoja na mambo mengine, huchambua habari za wasanii na kufanya nao mahojiano. Mwandishi pia amekuwa akifuatilia kwa karibu habari za wasanii na sanaa ya BF kupitia vyanzo mbalimbali vya habari. Wasanii waliomakinikiwa na kutumiwa kama sampuli ni wale wanaoimba muziki wa R & B, Zuku, Hip-hop, na Injili. Makala haya yamebaini kuwa mambo yafuatayo yanayowafanya wasanii kuibuka na kung’ara katika BF: Kuwa na kipaji kizuri cha kuimba, kujituma, na udhamini au menejimenti nzuri. Kwa upande mwingine makala pia yamebaini kuwa wasanii hao hupotea katika tasnia ya muziki kwa sababu mbalimbali: Sababu za kiuelewa (kuelewa mambo mbalimbali), sababu za kiutandawazi na usasa, sababu za kielimu (elimu ya darasani), sababu za kimenejimenti, migogoro baina ya wasanii, na kuingia mgogoro na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA). Kutokana na matokeo hayo, mwandishi wa makala haya ameibua nadhariatete inayotawala mustakbali wa wasanii wa BF. Nadhariatete hii inaeleza

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.