Uhusiano wa Propaganda na Fasihi: Fasili, Maendeleo, na Mdhihiriko Wake

Authors

  • Wallace Mlaga Chuo Kikuu cha Rwanda

Abstract

Makala haya yanakusudia kujibu maswali kadhaa ya msingi yanayojitokeza wakati wa kujadili fasihi na propaganda. Miongoni mwa maswali hayo ni: Kuna uhusiano gani kati ya propaganda na fasihi? Je, kuna uhusiano gani kati ya propaganda na ushawishi? Propaganda katika kazi za fasihi zimejitokeza katika kipindi fulani tu cha wakati na baada ya hapo kukoma? Je, kila kazi ya fasihi ina upropaganda? Je, propaganda ni kitu kiovu na kisichopaswa kuhusishwa na fasihi? Je, katika zama hizi zinazojulikana kama zama za propaganda, fasihi imejitenga na propaganda au inaakisi? Mwisho, ni swali kuhusu propaganda inadhihirikaje katika matini ya kifasihi? Hivyo, majibu ya maswali haya yanafanikisha kueleza uhusiano uliopo baina ya propaganda na fasihi. Zaidi ya hayo, makala yanaonesha namna ambavyo historia ya fasihi haijawahi kujitenga na propaganda katika kipindi chochote cha wakati. Aidha, makala yanaonesha namna ambavyo propaganda siyo kitu kibaya kiasi cha kufikiriwa kuepuka kuhusishwa na fasihi. Mwisho, makala yanatoa mwongozo wa namna ya kubainisha mdhidhiriko wa propaganda katika matini za kifasihi. Hii inatoa nafasi pia ya kuepuka kutaja tu kuwa kazi fulani ya fasihi ina propaganda pasipo kutoa mifano dhahiri ya mbinu za kisanaa zilizotumika kupambanua propaganda hizo.

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biography

Wallace Mlaga, Chuo Kikuu cha Rwanda

Mwalim

Downloads

Published

2020-02-27

Issue

Section

Articles