Ruwaza ya Istilahi Ambatani katika Kiswahili: Mifano kutoka Istilahi Mkopo za Sayansi

Zabroni T. Philipo

Abstract


Kutokana na mkanganyiko wa ruwaza ya ‘istilahi ambatani’ (IA) uliopo baina ya watumiaji istilahi hizo na asasi zenye dhamana ya uundaji istilahi za Kiswahili, makala haya yameonesha ruwaza ya IA katika Kiswahili. Mbinu zilizotumika kupata data na hoja zilizowasilishwa katika makala haya ni udodosaji, usaili, na mapitio ya nyaraka1. Hivyo, mkanganyiko huo, unashadidia kuwa kuna uhalali wa kuangalia upya ruwaza ya IA katika Kiswahili. Makala haya yamebainisha kuwa ruwaza ya IA katika Kiswahili zenye elementi za sayansi, zifuate ruwaza inayozingatia kanuni za sayansi, ilhali istilahi ambatani za kawaida, zifuate mpangilio unaoongozwa na kanuni za sintaksia ya Kiswahili. Kwa kifupi, makala yanatoa mwongozo wa ruwaza za IA katika Kiswahili.

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.