Mizimu katika Ngano za Kiafrika: Uchambuzi wa Ngano Teule

Authors

  • Angelus Mnenuka University of Dar es salaam

Abstract

Fasihi simulizi ni sanaa inayotumia mbinu mbalimbali za kifani kujadili masuala anuwai katika jamii. Miongoni mwa mbinu za kifani zinazotumiwa kuyajadili masuala ya kijamii katika fasihi simulizi ni pamoja na matumizi ya wahusika wanaojulikana na watumiaji wa sanaa hiyo. Hii ina maana kwamba ili kufanikisha malengo yake, wahusika wanaosawiriwa katika fasihi simulizi mara nyingi wanajulikana kwa hadhira. Ingawa wahusika wengi wa fasihi simulizi hujulikana, baadhi hawaonekani katika jamii kwa kutumia milango mitano ya fahamu. Swali kuu ambalo linajadiliwa katika makala haya ni: Je, wahusika kama vile mizimu ambao hawaonekani kwa kutumia milango ya fahamu wanasawiriwaje katika fasihi simulizi? Katika makala haya tunachunguza usawiri wa mizimu katika ngano kwa kutumia Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Kimsingi, lengo kuu la makala haya ni kuonesha uhusiano uliopo baina ya mizimu katika ngano na Ontolojia ya Kiafrika. Kwa kuzingatia nduni bainifu za mizimu kama zilivyojadiliwa na wanazuoni mbalimbali, tumebaini kuwa mizimu, yaani wahenga na mazimwi ni dhana zilizochopolewa katika imani za Kiafrika, yaani ni sehemu ya Ontolojia ya Kifrika. Uhusiano baina ya mizimu yenyewe, na uhusiano baina ya mizimu na binadamu kimamlaka katika ngano unaweza kufafanuliwa vizuri kwa kutumia Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Kwa hiyo, ontolojia ya jamii ni msingi katika uhakiki wa kazi za fasihi, kwa sababu wahusika pamoja na usawiri wao huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo wa jamii kuhusu wahusika na uhusiano baina ya wahusika.

Downloads

Published

2021-08-17

Issue

Section

Articles