Mtindo na Wahusika katika Diwani za Dhifa na Wasakatonge
Abstract
Makala haya yamechunguza mtindo na wahusika katika diwani teule za Kiswahili ambazo ni Dhifa (2008) na Wasakatonge (2004). Data za msingi za makala haya zilikusanywa kutoka katika diwani teule kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini. Uchambuzi na mjadala wa data zilizowasilishwa ulifanywa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Simiotiki. Makala yanahitimisha kwamba diwani teule zina utajiri mkubwa uliojilimbikiza katika vipengele vya kimtindo na wahusika. Vipengele hivi hutumika kama nyenzo muhimu ya kisanaa kulingana na muktadha na utamaduni wa jamii inayohusika. Hitimisho hili linazidi kusisitiza msimamo kuwa fasihi hutegemewa kusawiri hali halisi iliyopo katika jamii kwa kuwa inafungamana na muktadha wa mifumo mahususi iliyopo katika jamii. Kwa mtazamo huo, fasihi inatumika kama chombo kinachomudu mazingira na harakati za kijamii kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisanaa, ikiwamo mtindo na wahusika.Downloads
Download data is not yet available.