Njia za Usawirishwaji wa Sihiri kwenye Utendi wa Rukiza na Dhima zake katika Kumpambanua Shujaa wa Kiutendi

Christopher B. Lucas, Ramadhani T. Kadallah

Abstract


Makala haya yamejihusisha na jinsi sihiri ilivyosawiriwa katika utendi wa Rukiza. Aidha, uchunguzi huu umechochewa na kuwapo kwa mgongano wa hoja baina ya wataalamu kuhusu matumizi ya sihiri katika kumjenga shujaa na kupambanua vipengele vingine vya kiutendi katika fasihi ya Kiafrika. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa njia ya maktaba na ilichambuliwa kwa kuzingatia mkabala wa kitaamuli. Kadhalika, Nadharia ya Uhalisia Mazingaombwe ndiyo iliyotumika kama dira ya kufikia matokeo ya utafiti huu. Matokeo yaliyopatikana baada ya uchambuzi wa data yanaonyesha kwamba sihiri husawiriwa kwa kutumia njia mbalimbali kama vile miujiza, sadaka, ramli, siri, nguvu za ajabu na ndumba. Kutokana na matokeo hayo, imehitimishwa kwamba sihiri ni kipengele muhimu sana katika fasihi ya Kiafrika, hasa katika tendi kwa kuwa pamoja na mambo mengine husaidia kupambanua nduni mbalimbali walizonazo mashujaa. Kushamiri kwa matumizi ya sihiri katika tendi kunadhihirisha jinsi ambavyo fasihi hususan tendi zinavyofungamana na tamaduni za Kiafrika

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.