Uchanganuzi wa Miundo ya Aristotle katika Tamthilia ya Kinjeketile

Richard Wafula, Pamela Ngugi, Sophie Okwena

Abstract


Makala haya yanalenga kuweka wazi miundo ya Aristotle katika tamthilia ya Kinjeketile (1969). Kinjeketile ni tamthilia ya Kiswahili ambayo iliandikwa mwishoni mwa miaka ya 1960 wakati ambapo maigizo mengi yalichukua miundo ya Kimagharibi moja kwa moja. Huu ni wakati ambapo Waingereza walileta drama kwa madhumuni ya kujifurahisha wao wenyewe na kujikumbusha maisha ya kwao. Katika kufanya hivi, waliwatumia Watanzania hasa, watoto wa shule katika kuonesha tamthilia za akina Aristotle. Watanzania waliathiriwa kiasi cha kuweza kujishirikisha kikamilifu katika kutunga tamthilia na kuzionesha. Ebrahim Hussein aliandika Kinjeketile akitumia miundo ya kina Aristole, hasa tanzia ya Kigiriki ambayo hasa ndiyo msingi wa sheria za ki-Aristotle. Kutokana na masomo yake, Hussein aliweza kuiga miundo ya Aristotle katika utunzi wake

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.